• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Misri, Ethiopia na Sudan zakutana mjini Khartoum kujadili suala la bwawa la Nile

    (GMT+08:00) 2018-04-05 08:48:31

    Ujumbe kutoka Misri na Ethiopia umewasili nchini Sudan kushiriki kwenye mkutano wa pande tatu kuhusu mradi wa bwawa la Renaissance la Ethiopia GERD.

    Waziri wa Mambo ya nje wa Sudan Bw Ibrahim Ghandour na waziri wa maji na Umeme Bw Mutaz Mussa waliukaribisha ujumbe wa Misri na Ethiopia kwenye mkutano huo.

    Mkutano huo unatarajiwa kupitia njia za matumizi ya maji ya mto Nile na kufanya Bwawa la Renaissance kunufaisha maendeleo ya kila nchi, badala ya kuwa chanzo cha mgogoro. Mkutano uliopita kuhusu matumizi ya maji ya mto Nile haukuwa na mafanikio baada ya pande husika kutofikia makubaliano.

    Misri ina wasiwasi kuwa bwawa la Renaissance litapunguza mgao wake wa maji kutoka mto Nile, na Ethiopia inaona kuwa bwana hilo litailetea maendeleo makubwa ya kiuchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako