• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uturuki, Russia na Iran zafikia makubaliano kuhusu ufumbuzi wa kisiasa wa suala la Syria

    (GMT+08:00) 2018-04-05 08:57:45

    Marais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki, Vladimir Putin wa Russia na Hassan Rouhani wa Iran wamekutana mjini Ankara, Uturuki, na kufikia makubaliano mengi kuhusu ufumbuzi wa kisiasa wa suala la Syria.

    Baada ya mkutano huo, nchi hizo tatu zimetoa taarifa ya pamoja ikisema kuwa, ufumbuzi wa kisiasa ni njia pekee yenye ufanisi ya kutatua mgogoro wa Syria, na matumizi ya nguvu hayataweza kutatua mgogoro huo.

    Nchi hizo tatu pia zimesisitiza kuwa zinapinga hatua za kuchochea mfarakano wa Syria kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi, na kuahidi kulinda kithabiti mamlaka, uhuru na ukamilifu wa ardhi wa Syria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako