• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bunge la Botswana laidhinisha makamu mpya wa rais

    (GMT+08:00) 2018-04-05 08:58:10

    Bunge la Botswana limeidhinisha mbunge kutoka chama tawala cha nchi hiyo Bw. Slumber Tsogwane kuwa makamu wa rais wa nchi hiyo.

    Bw. Tsogwane aliteuliwa na rais mpya wa nchi hiyo Bw. Mokgweetsi Masisi tarehe 1 Aprili. Kati ya wabunge 54 ambao walikuwa na haki ya kupiga kura, 35 walipiga kura za ndio huku mmoja akipiga kura ya hapana.

    Wabunge wengi wa vyama vya upinzani walisusia kupiga kura na wengine hawakupiga kura kabisa.

    Baada ya kuapishwa kuwa rais mpya, Bw Masisi aliachia nafasi yake ya uenyekiti wa chama na kumteua Bw. Tsogwane kuchukua nafasi yake, kitendo ambacho kimeungwa mkono na kamati kuu ya chama.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako