• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • ZFA yatoa adhabu kwa timu tatu Zanzibar

    (GMT+08:00) 2018-04-05 09:03:26
    Chama cha mpira wa miguu Zanzibar (ZFA) kimetoa adhabu kwa timu tatu zinazoshiriki ligi kuu Zanzibar kanda ya Unguja kwa kosa la kuingia uwanjani kupitia mlango usiostahili kuingia wachezaji uwanjani.

    Adhabu hiyo imetolewa kwa timu ya Black Sailors, Miembeni City na Kilimani City ambapo kila timu inatakiwa kulipa faini ya shilingi laki moja kwa kosa hilo.

    Kwa upande mwiginge ZFA imemuadhibu kocha msaidizi wa timu ya Kilimani City Abrahamani Mussa kutokaa katika benchi la ufundi kwa muda usiojulikana kutokana na kutoa lugha chafu kwa waamuzi waliochezesha mchezo kati ya Kilimani City dhidi ya Black Sailors.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako