• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Zimbabwe zakubaliana kuimarisha ushirikiano maeneo muhimu

    (GMT+08:00) 2018-04-05 09:16:03

    China na Zimbabwe zimekubaliana kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana katika maeneo muhimu, na kuinua kiwango cha uhusiano kati yao.

    Makubaliano hayo yamefikiwa wakati wa mkutano kati ya waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang na rais wa Zimbabwe Bw. Emmerson Mnangagwa.

    Bw. Li amesema China itaendelea kutekeleza kanuni za udhati, urafiki na usawa, na kuleta nguvu mpya kwenye urafiki wa jadi kati ya China na Zimbabwe. Amesema China iko tayari kushirikiana na Zimbabwe kupanua njia za ushirikiano katika ujenzi wa miundombinu, kilimo, uwezo wa uzalishaji na raslimali watu.

    Kwa upande wake Rais Mnangagwa amesema serikali ya Zimbabwe imejitolea kuimarisha urafiki wa jadi na China, na kukuza ushirikiano wa kunufaishana katika maeneo kama vile biashara, miundombinu, nishati, kilimo na utalii, ili kuinua uhusiano kati ya nchi mbili ufikie kwenye ngazi mpya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako