• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa walaani mashambulizi dhidi ya Tume ya Umoja wa Afrika nchini Somalia

    (GMT+08:00) 2018-04-05 09:16:26

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani mashambulizi ya kigaidi dhidi ya askari wa Uganda wa Tume ya Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM, ambayo yalisababisha vifo na majeruhi kwa askari hao.

    Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa wametoa taarifa wakionesha kusikitishwa na kutoa rambirambi kwa serikali ya Uganda na familia za wahanga, na kuwatakia waliojeruhiwa wapone haraka. Baraza limesisitiza kuwa linaiunga mkono kikamilifu AMISOM ili kupunguza tishio la kundi la kigaidi la Al-Shabaab na makundi ya upinzani nchini Somalia.

    Wapiganaji wa kundi la Al-Shabaab waliokuwa wamesheheni silaha nzito walishambulia kambi ya tume ya AMISOM na kulipua magari mawili na kupambana kwa saa kadhaa. AMISOM imesema imepoteza askari wake wanne.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako