• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa UN amteua kamanda mpya wa tume ya Umoja wa Mataifa huko Abyei

    (GMT+08:00) 2018-04-05 09:32:44

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw Antonio Guterres ametangaza kumteua Meja Jenerali Gebre Adhana Woldezgu kutoka Ethiopia kuwa kamanda mpya wa tume ya Umoja wa Mataifa huko Abyei, eneo linalogombewa kati ya Sudan na Sudan Kusini.

    Bw Gebre amechukua nafasi ya Meja Jenerali Tesfay Gidey Hailemichael wa Ethiopia, ambaye amesifiwa kutoa mchango mkubwa kwa tume hiyo.

    Akizungumza na wanahabari Bw Guterres amesema Bw Gebre ana uzoefu wa miaka 38 katika jeshi la Ethiopia, na amewahi kwenda mara kwa mara Sudan, Sudan Kusini, Kenya, Uganda na tume ya Umoja wa Mataifa nchini Somalia, kwa ajili ya kuimarisha uratibu wa mambo ya usalama na mipaka. Aidha, amewahi kushiriki kwenye kazi ya upangaji wa operesheni za kulinda amani za kimataifa na za kikanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako