• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Burundi yashutumu Rwanda na wafanyakazi wa UNHCR kuwateka nyara wakimbizi wa Burundi

    (GMT+08:00) 2018-04-05 09:33:03

    Serikali ya Burundi imeishutumu Rwanda na wafanyakazi wa Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR kwa kuwateka nyara wakimbizi wa Burundi.

    Msemaji wa serikali ya Burundi Bw Philippe Nzobonariba ametoa taarifa akiihimiza Rwanda kuwaachia huru na kuwarejesha wakimbizi wanaoshikiliwa mateka na serikali ya Rwanda kwa kushirikiana na wafanyakzi wa ofisi ya Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa nchini Rwanda.

    Taarifa hiyo imetolewa baada ya kurejeshwa kwa takriban wakimbizi 2,500 kutoka kambi tatu za mpito nchini Rwanda wikiendi iliyopita.

    Tarehe 31 mwezi Machi, wizara ya mambo ya maafa na wakimbizi ya Rwanda imesema wakimbizi zaidi ya 2,500 wa Burundi walioingia Rwanda kutoka kambi moja ya DRC, watarejeshwa Burundi kuanzia tarehe 1 mwezi huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako