• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yachukua hatua kukabiliana na kitendo cha kujilinda kibiashara cha Marekani

    (GMT+08:00) 2018-04-05 18:37:53

    Saa 11 baada ya Marekani kutangaza orodha ya bidhaa za China zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 50 zitakazoongezewa ushuru wa forodha, China imetoa orodha ya bidhaa za Marekani zitakazoongezewa ushuru wa forodha ili kulipiza kisasi. Bidhaa hizo ni pamoja na soya, magari na ndege ambazo ni muhimu kwa Marekani.

    Orodha hiyo ya China imetolewa baada ya kuchambuliwa na kutathminiwa na wataalamu, na itatekelezwa rasmi mara baada ya Marekani kuanza kuongeza ushuru wa forodha kwa bidhaa za China.

    Jibu hili la China halikutarajiwa na watu wengi. Katika mivutano ya zamani ya biashara kati ya Marekani na nchi nyingine, mshindani wake hakufanya kama China ilivyofanya.

    Kwanza, China ina msimamo thabiti. Zamani Japan na nchi za Ulaya hazikuthubutu kulipiza kisasi Marekani moja kwa moja. Hata hivyo China imefanya mazungumzo ya kutosha na Marekani kabla ya kuchukua hatua hiyo.

    Pili, China imechukua hatua kwa haraka. Hatua hiyo ambayo haikutarajiwa na pande nyingi imeiogopisha Marekani.

    Tatu, China imechukua hatua inayofaa. China imeweka bidhaa muhimu za Marekani zikiwemo soya, magari na ndege kwenye orodha ya bidhaa zitakazoongezewa ushuru wa forodha.

    Soko lina busara. Mara baada ya China kutangaza orodha ya bidhaa za Marekani zitakazoongezewa ushuru wa forodha, soko la hisa limeanguka kwa karibu asilimia 2.

    Ili kutuliza soko la hisa, rais Donald Trump amesema Marekani haifanyi vita ya biashara na China, kwani Marekani imeshindwa katika vita hiyo miaka mingi iliyopita.

    Waziri wa biashara wa Marekani Wilbur Ross amesema, bado kuna uwezekano wa kutatua mvutano wa biashara na China kwa njia ya mazungumzo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako