• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani yasema hakuna muda rasmi wa vikosi vyake kuondoka nchini Syria

    (GMT+08:00) 2018-04-05 19:35:10

    Ikulu ya Marekani imesema kuwa hakuna muda rasmi uliopangwa kwa vikosi vya nchi hiyo kuondoka nchini Syria, ingawa rais wa Marekani ameonyesha nia ya kuondoa haraka jeshi la nchi hiyo nchini Syria.

    Msemaji wa ikulu ya Marekani Sarah Sanders amesema, rais Donald Trump wa nchi hiyo anaangalia uwezekano wa kushinda vita hiyo kihalisi, na sio kuweka idadi kubwa ya askari nchini Syria.

    Wakati huohuo, wizara ya ulinzi ya Marekani na wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo zimeeleza wasiwasi wao kuwa juhudi za muda mrefu zinahitajika ili kulishinda kikamilifu kundi la wapiganaji la IS.

    Mpaka sasa, jumla ya askari 2,000 wa Marekani wako nchini Syria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako