• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wananchi wakumbatia teknolojia ibuka nchini Rwanda

    (GMT+08:00) 2018-04-05 19:46:24

    Kasi ya ukumbatiaji wa teknolojia mpya nchini Rwanda imeongezeka katika miaka ya hivi karibuni,na kuboresha maisha ya watumizi.

    Watu wengi sasa hata wa vijijini wanaweza kulipia chakula katika masoko na hata nauli ya bodaboda kwa kupitia simu za mkononi.

    Hii imetokana na ushirikiano kati ya benki na kampuni za simu za mkononi ambapo kupitia programu maalum wateja wanaweza kufanya malipo ya manunuzi yao.

    Hii inawawezesha wafanyabaishara wenye maduka,migahawa,baa,vibanda vya chakula,teksi kukubali malipo kutoka simu za mkononi bila kuwa na vifaa vingine.

    Kwa kuanzisha teknolojia kama hizi,benki pamoja na taasisi nyengine za fedha zinalenga kuvutia wateja wapya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako