• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Tanzania kutekeleza kilimo cha vitalu nyumba katika kila halmashauri

    (GMT+08:00) 2018-04-05 19:46:43

    Serikali ya Tanzania imesema kupitia awamu ya pili ya programu ya kuendeleza sekta ya kilimo imeandaa mradi wa kilimo cha kutumia vitalu nyumba utakaotekelezwa kwa kila halmashauri nchini.

    Hayo yalielezwa jana bungeni na Naibu Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) ,Joseph Kakunda,alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Madaba Joseph Mhagama.

    Mbunge huyo alitka kujua mpango wa serikali wa kuwajengea uwezo wakulima na wafugaji ili kuendesha shughuli zao katika maeneo madogo lakini kwa tija kubwa na kuwaondolea adha wanazozipata.

    Akijibu swali hilo,Kakunda alisema halmashauri hizo zitajenga vitalu nyumba visivyopungua viwili ili kusambaza teknolojia mpya ya kilimo kwa wananchi.

    Aidha alisema hadi kufikia disemba mwaka 2017 kuna maafisa ugani 13,532 nchini na kati yao maofisa ugani 8,232 ni wa kilimo cha mazao 4,283 ni wa mifugo ,493 ni wa uvuvi na 524 ni wa ushirika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako