• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapinga kithabiti matumizi ya silaha za kemikali katika mazingira yoyote

    (GMT+08:00) 2018-04-05 19:49:44

    Naibu balozi wa China katika Umoja wa Mataifa Bw. Wu Haitao jana amesema, China inapinga kithabiti nchi na jumuiya yoyote, au mtu yeyote kutumia silaha za kemikali kutokana na mazingira yoyote, pia amesisitiza kuwa njia ya kisiasa ni utatuzi pekee wa suala la Syria.

    Bw. Wu Haitao ameyasema hayo katika mjadala wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu suala la matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria. Amesema, China siku zote inafuatilia na kulaani vikali mashambulizi yoyote dhidi ya raia, na msimamo wa China kuhusu suala la silaha za kemikali ni kupinga kithabiti matumizi ya silaha hizo. China inaunga mkono kufanya uchunguzi wa haki kwa pande zote kuhusu tukio la matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria, ili kupata matokeo ya kweli, na kuwakamata wahusika wanaotumia silaha hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako