• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maseneta wa Rwanda waunga mkono ombi la kuorodhesha majengo ya mauaji ya kimbari kwenye Urithi wa UNESCO

    (GMT+08:00) 2018-04-06 08:45:33

    Maseneta nchini Rwanda wameidhinisha hatua ya nchi yao ya kuomba kuorodhesha majengo manne ya mauaji ya kimbari kikiwemo Kituo cha Kumbukumbu cha Mauaji ya Kimbari cha Kigali kwenye maeneo ya Urithi wa Dunia wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO. Akizungumza kwenye mkutano wa kujadili ombi hilo uliofanyika bungeni mjini Kigali, mwenyekiti wa Baraza la Seneti Bw. Bernard Makuza amesema hatua hiyo inaweza kuelimisha dunia kuhusu historia ya Rwanda na kuzuia mauaji kama hayo yasitokee tena duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako