• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania Yateuliwa kuwa mwenyeji wa mashindano ya kujihami

  (GMT+08:00) 2018-04-06 09:09:42

  Tanzania imechaguliwa kuwa mwenyeji wa mashindano ya mchezo wa kujihami yaani (Tae kwo-ndo) kwa nchi za Afrika Mashariki yatakayofanyika mwezi mei mwaka huu.

  Rais wa Tae kwo-ndo kwa nchi za Afrika Mashariki, Kennedy Said amesema jana kuwa maandalizi ya mashindano hayo yameanza na yatakutanisha wachezaji zaidi ya 70 kutoka nchi za Uganda, Burundi, Kenya, Rwanda na wenyeji Tanzania.

  washindi wa mashindano hayo watapata nafasi ya kushiriki fainali ya kuwania ubingwa wa mchezo huo Afrika utakaofanyika Addis Ababa, Ethiopia Agosti mwaka huu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako