• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yachangia kompyuta kwa chama tawala cha Sudan Kusini SPLM

    (GMT+08:00) 2018-04-06 09:24:34

    Ubalozi wa China nchini Sudan Kusini umetoa kompyuta 38 kwa chama tawala cha nchi hiyo SPLM, ili kuunga mkono shughuli zake. Balozi mdogo wa China nchini humo Bw. Liu Xiaodong amesema nchi hizo mbili zinasaidiana kwenye nyanja mbalimbali, na kuongeza kuwa China inapenda kubadilishana uzoefu wa mafanikio yake na Sudan Kusini.

    Pia ameutaka uongozi wa chama hicho kuharakisha ugavi wa kompyuta hizo ili kuunganisha makao makuu ya chama hicho na maofisa wake kote nchini. Kaimu katibu mkuu wa chama cha SPLM Bw. Jema Nunu Kumba amesema, msaada huo utasaidia kurahisisha uendeshaji wa chama chake nchini Sudan Kusini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako