• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Trump atishia kuongeza ushuru wa dola bilioni 100 za kimarekani dhidi ya bidhaa za China

    (GMT+08:00) 2018-04-06 09:25:10

    Rais Donald Trump wa Marekani ametisha kuongeza ushuru wa dola bilioni 100 za kimarekani dhidi ya bidhaa za China.

    Rais huyo amesema kutokana na kitendo cha kulipiza kisasi cha China, ameamuru ofisi ya mwakilishi wa biashara wa Marekani kufikiria uwezekano wa kuonegza ushuru wa ziada wa dola bilioni 100 za kimarekani dhidi ya bidhaa China.

    Wakati huohuo, wadau wa biashara nchini Marekani wamezitaka serikali za nchi hizo mbili kutatua mvutano wa kibiashara kwa njia ya mazungumzo.

    Mwenyekiti wa chama cha wakulima wa soya cha Marekani Bw. John Heisdorffer ametoa taarifa akiitaka serikali ya Trump kuchukua msimamo wa kiujenzi kutatua mvutano huo na China badala ya kuchukua hatua ya adhabu, ili kuepusha hasara kwa wakulima wa soya wa Marekani.

    Kampuni ya General Motors ya Marekani pia imetoa taarifa ikisema, inaunga mkono uhusiano mzuri wa kibiashara kati ya China na Marekani, huku ikizitaka serikali za nchi hizo mbili kuendelea na mazungumzo ya kiujenzi na kuhimiza sera endelevu za kibiashara.

    Kampuni ya Ford ya Marekani imesema inazihimiza serikali za nchi mbili kufanya juhudi za pamoja ili kutatua mvutano wa kibiashara. Kampuni ya Boeing ya Marekani pia imetoa taarifa kuwataka viongozi wa nchi hizo mbili kufanya mazungumzo ya kiujenzi, huku ikiendelea kufanya juhudi kuwasiliana na serikali za pande mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako