• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yasema uwekezaji wa China ni muhimu kwenye kufanikisha ajenda ya maendeleo ya viwanda

    (GMT+08:00) 2018-04-06 09:30:23

    Kenya imesema inapenda kutumia mitaji na teknolojia kutoka makampuni ya China, ili kuhimiza maendeleo ya viwanda ambayo ni moja ya ajenda nne kubwa za serikali ya Rais Uhuru Kenyatta.

    Waziri asiye na wizara maalum na katibu mkuu wa chama tawala cha Jubilee Bw Raphael Tuju amesema Kenya imeweka mazingira mazuri ya kuvutia uwekezaji zaidi kutoka China kwenye sekta ya viwanda, na ni muhimu kwa Kenya kushirikiana na China na kuendeleza sekta ya viwanda, ambayo ni muhimu kwa maendeleo na kuwapatia ajira vijana wasio na ajira.

    Akiongea kwenye ziara ya kiwanda cha kutengeneza marumaru kinachomilikiwa na wachina cha Twyford, kilichoko kwenye eneo la Kajiado, Bw Tuju amesema uwekezaji wa kiwanda hicho unaokadiriwa kuwa na thamani ya dola za kimarekani milioni 80 umeinua hadhi ya Kenya ya kituo cha uzalishaji.

    Ofisa wa ubalozi wa China aliyeambatana na Bw Tuju kwenye ziara hiyo Bw. Wang Xuezheng amesema China inapenda kuwa sehemu ya juhudi za kuendeleza sekta ya viwanda ya Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako