• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalamu wa Afrika wajipanga kutafuta teknolojia za kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa

    (GMT+08:00) 2018-04-06 09:30:42

    Wawakilishi kutoka serikali za nchi za Afrika, sekta binafsi, taasisi za fedha na utafiti wanapanga kukutana nchini Kenya kujadili ushirikiano na usafirishaji wa teknolojia, ili kusaidia kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa.

    Bw. Jukka Uosukianen ambaye ni mkurugenzi wa kituo na mtandao wa teknolojia ya hali ya hewa cha Umoja wa Mataifa kinachoandaa mkutano huo, amesema mkutano huo unafanyika wakati Afrika inakabiliana na changamoto kubwa za mabadiliko ya hali ya hewa, ongezeko la ukame, mvua kubwa na mafuriko, ambazo zina athari kwenye usalama wa chakula.

    Bw Uosukianen amesema kituo chake kinahimiza maendeleo na usafirishaji wa teknolojia zisizosababisha uchafuzi, na kuzisaidia nchi zinazoendelea kupata teknolojia.

    Amesema kwa sasa teknolojia zaidi ya 100 ziko njiani kwenda kwenye nchi zaidi ya 75 duniani, zikiwa ni za sekta za kilimo, nishati, viwanda na usafirishaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako