• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China haiogopi Marekani kuongeza bidhaa za kuongezewa ushuru wa forodha

  (GMT+08:00) 2018-04-06 17:43:03

  Rais Donald Trump wa Marekani jana alitoa taarifa akisema amewaagiza wajumbe wa biashara wa nchi hiyo kufikiria kuongeza bidhaa za China zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 100, kwenye orodha za bidhaa zitakazoongezewa ushuru wa forodha. Mkuu wa idara ya utafiti wa uchumi wa kimataifa ya taasisi ya utafiti wa masuala ya kimataifa ya China Bw. Jiang Yuechun amesema, China haitatishwa na vitendo vya kimabavu vya Marekani katika mambo ya biashara.

  Bw. Jiang amesema, kuweka vikwazo vya biashara kunadhuru maslahi ya pande mbili, mvutano wa kibiashara unakiuka kanuni ya kimsingi ya uchumi, na utaratibu wa biashara huria duniani. Marekani ikiwa nchi kubwa zaidi iliyoendelea, sekta yake huduma inachukua zaidi ya asilimia 70 ya uchumi. Na China ni nchi kubwa zaidi inayoendelea na yenye idadi kubwa ya watu duniani, inatengeneza bidhaa zenye faida ndogo na kuziuza katika nchi za nje. Hivi sasa ukosefu wa uwiano wa biashara unatokana na mgawanyiko wa kazi, miundo tofauti wa uchumi, na njia ya mahesabu, haupaswi kutatuliwa kwa njia ya vizuizi.

  Bw. Jiang amesema kuweka vizuizi hakuwezi kubadilisha mkakati wa maendeleo ya nchi nyingine. Kwa mujibu wa orodha iliyotolewa na Marekani ya bidhaa za China zitakazoongezewa ushuru wa forodha, tunaweza kujua kuwa lengo la Marekani si kama tu ni utatuzi wa ukosefu wa uwiano wa biashara, bali pia ni kuzuia mpango wa kimkakati wa China wa uzalishaji wa mwaka 2025, ambao ni kwa ajili ya kuhimiza maendeleo ya sayansi na teknolojia ya hali ya juu.

  Katika historia, Marekani ilizifanyia nchi nyingine mara nyingi ukaguzi kwa mujibu wa kifungu cha 301 cha sheria yake ya biashara, lakini China ni tofauti na nchi nyingine. China ina ardhi kubwa na watu wengi, marekebisho ya muundo wa uchumi wa China hayatakatika kutokana na mvutano wa kibiashara iliozushwa na Marekani, na mpango wa uzalishaji wa mwaka 2025 pia hautakomeshwa na mgogoro huo. China itashinda shinikizo la nje, na kupata maendeleo zaidi ya uchumi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako