• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Russia yasema, wapiganaji elfu 8 wamehamishwa kutoka Syria kwenda Afghanistan

    (GMT+08:00) 2018-04-06 19:20:01
    Naibu mkurugenzi wa idara ya usalama ya Russia Bw. Sergei Smirnov amesema, wapiganaji wapatao elfu 8 waliokuwa nchini Syria wamehamishiwa Afghanistan.

    Akishiriki kwenye mkutano wa 32 wa baraza la kikanda la kupambana na ugaidi la Jumuiya ya Ushirikiano wa Shanghai(SCO) mjini Tashkent, nchini Uzbekistan, Bw. Smirnov amesema, wapiganaji hao wakiwemo wa kundi la IS, ni tishio la usalama kwa nchi wanachama wa SCO. Nchi hizo zimeamua kushirikiana kwa pamoja na kuchukua hatua kupunguza tishio hilo kadiri ziwezavyo, ambazo ni kubadilishana habari za wapiganaji na kuzuia wapiganaji hao kuingia kwenye nchi hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako