• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuongeza nguvu ya kulipiza kisasi kama Marekani kuongeza bidhaa za China zitakazoongezewa ushuru wa forodha

    (GMT+08:00) 2018-04-06 21:20:15

    Msemaji wa wizara ya biashara ya China Bw. Gao Feng amesema, kama Marekani ikitangaza orodha ya bidhaa mpya za China zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 100 zitakazoongezewa ushuru wa forodha, China itaongeza nguvu ya kulipiza kisasi bila ya kusita.

    Rais Donald Trump wa Marekani ametoa taarifa akisema, mwakilishi wa biashara wa Marekani anafikiria uwezekano wa kuongeza ushuru wa ziada wa dola bilioni 100 za kimarekani dhidi ya bidhaa China, huku akiongeza kuwa Marekani bado inataka kufanya mazungumzo. Bw. Gao amesema, mvutano huo umesababishwa na upande mmoja wa Marekani, ambao uhalisi wake ni upande mmoja wa Marekani kupambana na pande mbalimbali za dunia na hatua ya kujilinda kibiashara ya Marekani inavuruga biashara huria duniani. China itaendelea kupanua mageuzi na ufunguaji wa mlango, kulinda mfumo wa biashara wa pande mbalimbali, kuhimiza uhuru na urahisi wa biashara na uwekezaji duniani.

    Bw. Gao Feng amekanusha China inafanya mazungumzo na Marekani kuhusu mvutano wa biashara kama maofisa wa Marekani walivyosema. Amesema hivi karibuni maofisa wa uchumi na biashara wa nchi hizo mbili hawakufanya mazungumzo yoyote kuhusu masuala ya biashara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako