• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Korea Kusini kusitisha kufuta ushuru kwa bidhaa za Marekani

    (GMT+08:00) 2018-04-07 17:13:18

    Korea Kusini imeliarifu Shirika la Biashara Duniani (WTO) matarajio yake ya kusitisha kufuta ushuru kwa baadhi ya bidhaa za Marekani zinazoingizwa nchini humo, ili kujibu hatua za kujilinda za Marekani dhidi ya vifaa vya nishati ya jua na mashine za kufua nguo za Korea Kusini.

    Korea Kusini imesema, imeamua kusitisha makubaliano ya kuondoa ushuru na majukumu mengine juu ya biashara ya Marekani chini ya Makubaliano Makuu ya Ushuru na Biashara ya Mwaka 1994.

    Mwezi Januari, Marekani iliamua kutoza ushuru wa asilimia 50 kwa mashine za kufulia nguo zilizoagizwa kutoka nje katika miaka mitatu ijayo, na kuweka ushuru wa asilimia 30 kwa vifaa vya nishati ya jua katika miaka minne ijayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako