• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Serikali ya Trump, endelee na maonyesho yako!

  (GMT+08:00) 2018-04-07 18:10:27

  Masoko matatu ya hisa mjini New York yote yalianguka kwa asilimia zaidi ya 2 siku ya Ijumaa baada ya serikali ya Marekani kusema kuwa inafikiria kuongeza ushuru dhidi ya bidhaa za China zenye thamani ya dola za Marekani bilioni 100 zinazoagizwa nchini humo, kauli ambayo imeongeza wasiwasi kwa wawekezaji.

  Rais Donald Trump wa Marekani, ambaye alikuwa mwendeshaji wa kipindi maalum cha televisheni, hajabadilisha tabia yake tangu aingie kwenye Ikulu ya Marekani. Katika mwaka mmoja uliopita, ingawa bado kuna nafasi kwenye baraza la mawaziri, lakini hii haikumzuia rais Trump kuwafukuza kazi mawaziri, akiwemo Steve Bannon aliyekuwa mshauri mwandamizi wa rais, James Comey aliyekuwa mkurugenzi wa Shirika la Upelelezi la Marekani na Rex Tillerson aliyekuwa waziri wa mambo ya nje.

  Mbali na kuwasumbua wenzake, serikali ya Trump pia inashambulia dunia nzima. Muda mfupi baada ya kuingia madarakani, wizara ya biashara ya Marekani ilianza uchunguzi wa kipengele cha 232 cha sheria ya biashara dhidi ya bidhaa za chuma cha pua na alumini zinazoagizwa kutoka nje, na pia kurekebisha makubaliano ya biashara huria yaliyofikiwa kati yake na washirika wake mbalimbali. Nchi nyingi kama vile nchi za Umoja wa Ulaya, Japan, Argentina na Mexico hazipendi kuikasirisha Marekani lakini zinataka kupata msamaha. Ndiyo maana, rais Trump alibadilisha kipengele cha 232 cha uchunguzi na kusitisha kutoza ushuru mkubwa dhidi ya bidhaa hizo zinazoagizwa kutoka baadhi ya nchi.

  Hata hivyo, uchunguzi wa kipengele hicho ni hatua ya kwanza tu, kilele kilikuwa ni serikali ya Marekani kuanza uchunguzi wa kipengele cha 301 cha sheria ya biashara dhidi ya China, na kudai moja kwa moja kushambulia mpango wa "Made in China 2025" wa China. Lakini cha kushangaza, serikali ya Marekani ni kuwa China imerudia msimamo wake kuwa haiogopi jambo kama hilo na itafanya kila iwezavyo kujibu hatua za Marekani.

  Inaonekana kuwa safari hii "kipindi maalumu cha televisheni" cha rais Trump kitashindikana: katika mwaka mmoja uliopita tangu aingie madarakani, uchunguzi dhidi ya madai ya Russia kuingilia uchaguzi mkuu wa Marekani unaambatana naye, sasa atawezaje kuwakabili wapiga kura wale waliomchagua ifikapo uchaguzi wa katikati ya muhula? Sheria ya kupunguza kodi imeifanya Marekani kubeba madeni ya zaidi ya dola za kimarekani trilioni 20 au 21, ambayo yataweza kuongezeka zaidi, ni sawa na ndoto kwa watu kutarajia kuwa Marekani inaweza kulipa madeni yake yote inayodaiwa. Cha muhimu ni kuwa kuongezeka kwa madeni ya Marekani hakika kutaathiri sifa ya dola ya Marekani. Kama hadhi ya fedha zake kuwa sarafu ya dunia itayumba, itakuwa ni hasara kubwa kwa Marekani.

  Hivi sasa, mkakati bora zaidi wa Marekani ni "kuficha uwezo wake na kusubiri muda wake", na kubana matumizi. Kwa mfano kubadilisha tabia mbaya ya kufuja pesa, kutocheza mchezo wa kuchuma pesa kwa pesa, kuonesha nguvu bora, kuinua ufanisi wa uzalishaji na kutoa huduma bora kwa watu wa dunia kwa kupitia njia ya ushindani wenye usawa, na kuelewana na wengine, vitendo hivyo ambavyo ni muhimu kwa nchi mbalimbali kuhimiza utandawazi na kupinga sera ya kujilinda kibiashara.

  Hata hivyo, cha kusikitisha ni kuwa Marekani imeingia kwenye njia yenye makosa. Kwa mfano, wakati China inajitahidi kuinua uwezo wake kwenye teknolojia ya juu, badala ya kutoa ushirikiano, Marekani inataka kutumia hadhi yake ya uongozi kuzuia maendeleo ya China kwa kupitia kuzusha migogoro ya kibiashara na hata kuanzisha vita ya biashara. Lakini kituo cha uvumbuzi cha dunia kinaelekea upande wa mashariki, jambo ambalo halitabadilika. China imelimbikiza msingi imara wa kiuchumi, serikali na mashirika ya kiraia yanaweza kutenga pesa nyingi kwenye sekta ya utafiti wa sayansi, na China imejenga mfumo kamili wa uzalishaji, ambapo kila mwaka wanafunzi milioni saba nane wanahitimu kwenye vyuo vikuu na kuwa na soko kubwa zaidi duniani la ndani.

  Inatarajiwa kuwa matunda mengi zaidi ya uvumbuzi yataonekana nchini China. Kuna msemo hapa China, ambao ni "kustawisha taifa kwa vitendo", hali ambayo China imekuwa nchi inayoomba hataza zaidi duniani kwa miaka mingi mfululizo imeonesha hali hiyo.

  Inaonekana kuwa serikali ya Trump haitaacha na kukiri kushindwa kwake wakati hata kipindi hiki kitakaposhindikana. Basi, endelee na maonyesho yako.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako