• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wachumi wa China wasema njia pekee ya kutatua mgogoro wa biashara kati ya China na Marekani ni kupigana nayo

    (GMT+08:00) 2018-04-07 21:22:07

    Jopo la Washauri Bingwa wa Biashara la China CF40 limekutana leo hapa Beijing na kusema kuwa mgogoro wa kiuchumi na kibiashara wa sasa kati ya China na Marekani umezushwa na Marekani, na njia pekee ya utatuzi ni kupigana nayo. Wataalamu hao wamesema wakati wa kukabiliana na changamoto hizo, China inajitahidi kufanya vizuri shughuli zake.

    Baada ya Marekani kutangaza kuongeza ushuru wa dola za kimarekani bilioni 50 dhidi ya bidhaa zinazoagizwa kutoka China nchini humo kwa mujibu wa uchunguzi wa kipengele cha 301 cha sheria ya biashara ya Marekani na kuona China kuchukua hatua za kuongeza ushuru dhidi ya bidhaa za Marekani, jana ilitangaza tena kuwa huenda itaongeza ushuru dhidi ya bidhaa za China zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 100. Hapo baadaye, China ilisema moja kwa moja kuwa itafanya kila iwezalo kujibu hatua hiyo ya Marekani.

    Mwanachama wa Jopo la CF40 Guo Kai amesema Marekani imeanzisha vita ya biashara kwa mujibu wa uchunguzi wa kipengele cha 301, na njia pekee ya utatuzi ni kupigana nayo.

    "Sababu ya kuanzisha vita hiyo ni uchunguzi wa kipengele cha 301, na kama ukisoma kwa makini ripoti ya uchunguzi huo, utafahamu kuwa mengi ya ripoti hiyo yamebuniwa nao, na wanayofikiria na wanayofanya hayana uhusiano, lengo ni kutoza ushuru tu. Vyombo vya habari vya Marekani pia vimeripoti kuwa Trump alisema 'sifikirii hakimiliki, ninachoangalia ni ushuru', kwa hiyo mgogoro wa biashara umezushwa na Marekani. Katika hali hiyo, njia pekee ni kupigana nayo mpaka iombe radhi. Serikali ya China imeonesha matarajio mara nyingi ya kufanya mazungumzo na Marekani, lakini Marekani hakuthamini. Tumefikia hatua hiyo, njia pekee ni kupigana nayo."

    Kabla ya hapo, serikali ya China imesisitiza mara nyingi na kuonya kuwa vita ya biashara haina mshindi. Kwa nini Marekani inapuuza na kuendelea kuchukua hatua? Baada ya uhusiano kati ya dola ya Marekani na dhahabu kutenganishwa, utaratibu wa kujirekebisha wa uchumi wa Marekani umeharibiwa, na biashara ya Marekani na nchi za nje imekuwa ikishuhudia urari mbaya tokea mwaka 1975. Hii ni hali halisi inayogunduliwa na watalamau na watafiti wengi.

    Kuhusu urari mbaya wa biashara ya Marekani na nchi za nje, mtafiti wa ngazi ya juu wa Jopo la CF40 Ha Jiming amaeleza sababu nyingine kadhaa.

    "tokea China ianze kutekeleza sera ya mageuzi na ufunguaji mlango, haswa baada ya kujiunga na Shirika la Biashara Duniani WTO, makampuni mengi ya nchi za nje yamekuja China kuanzisha viwanda, kwa hivyo China ikabadilika kuwa kiwanda cha dunia, na kusababisha bidhaa nyingi zina thamani ndogo ya nyongeza nchini China, lakini kwenye biashara ya kimataifa, bidhaa hizo zinahesabiwa kuwa ni urari mzuri wa biashara ya China na nje. Marekani inazuia kuuza baadhi ya bidhaa zake nje ya nchi, haswa zile zenye teknolojia ya juu. Kama Marekani inaweza kuruhusu bidhaa za teknolojia ya juu kuuzwa nchini China, naona pengo la biashara kati ya China na Marekani litapungua kidhahiri na kwa kasi."

    Bw. Ha anaona kuwa kuongeza ushuru hakusaidia hata kidogo Marekani kupunguza urari mbaya wa biashara yake na nchi za nje, na matokeo ni kuwa bidhaa zitakazoagizwa kutoka China zitapungua na zitakazoagizwa kutoka nchi nyingin kuongezeka tu. Kuongeza ushuru ovyo na kuanzisha vita ya biashara kutaipa hasara Marekani yenyewe.

    Naye mtafiti wa ngazi ya juu wa jopo hilo la CF40 Guan Tao anasisitiza kuwa nguvu bora zaidi ya China ni kuwa ina soko kubwa la kutosha, na China inatoa mchango kwa mfumo wa biashara wa pande nyingi duniani kwa kutegemea soko lake.

    "Naona China haipendi kushiriki kwenye vita ya biashara, na Marekani inailazimisha kushiriki. China ina soko kubwa, na tunachofanya ni kufungua zaidi soko la China na kuziruhusu nchi nyingi kunufaika na ukuaji wa uchumi wa China. Huu ni mchango unaotolewa na China kwa mfumo wa biashara wa pande nyingi duniani."

    China imeeleza wazi kuwa itafanya kila iwezalo na kuchukua hatua kabambe kujibu vitendo vya Marekani vya kuongeza ushuru na kutoa tishio kwa lengo la kukwamisha maendeleo ya China, ili kulinda maslahi ya taifa na wananchi wake. Kwa upande mwingine, China itaendelea kutekeleza sera ya mageuzi na ufunguaji mlango, kulinda mfumo wa biashara ya pande nyingi, na kuhimiza uhuru na urahisi wa biashara duniani.

    Mwanachama wa jopo la CF40 Peng Wensheng anaona kuwa katika kukabili changamoto hizo, China inajitahidi kufanya shughuli zake.

    "China inatakiwa kufanya vizuri shughuli zake. Kama ilivyosema ripoti ya serikali, itapunguza kwa kiasi kikubwa mapato ya nyongeza ya sekta ya uzalishaji. Tukitaka kubadilisha mambo mabaya kuwa mambo mazuri, kwanza tunatakiwa kufanya vizuri shughuli zetu."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako