• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watatu wafariki, wengine wakijeruhiwa kutokana na shambulio la kugongwa na gari

    (GMT+08:00) 2018-04-08 16:38:05

    Watu watatu akiwemo dereva mmoja aliyehusika wamefariki na wengine kadhaa wakijeruhiwa, baada ya gari kuparamia kusanyiko la watu kwenye mji mkongwe wa Muenster ulioko magharibi ya Ujerumani.

    Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari waziri wa eneo la Rhine-Westphalia Herbert Reul, ameeleza kuwa dereva mmoja aliyekuwa akiendesha gari aina ya Volkswagen aligonga kundi la watu waliokuwa wamekaa kwenye viti vya nje ya mgahawa kwenye mji wa Muenster, akifafanua kuwa dereva huyo ambaye alijiua kwa bastola baada ya kusababisha maafa anadhaniwa kuwa na tatizo la kiakili.

    Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ameeleza kushtushwa na shambulio hilo akisema kuwa serikali inafanya kila liwezekanalo ili ukweli ujulikane na kuwasaidia wahanga pamoja na ndugu zao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako