• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Zimbabwe arejea nyumbani baada ya ziara yake nchini China

    (GMT+08:00) 2018-04-08 16:38:50

    Rais wa Zimbabwe Emerson Mnangagwa jana jumamosi amewasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Harare baada ya kukamilisha ziara ya siku tano nchini China.

    Kabla ya kuondoka nchini China Rais Mnangagwa aliandika katika ukurasa wake wa Facebook kuwaambia Wazimbabwe kuwa mafanikio mengi yamepatikana kutokana na ziara yake hiyo.

    Mnangagwa amesema kuwa alifanya mikutano mingi itakayozaa matunda, na wafanyabiashara pamoja na viongozi mbalimbali wa kisiasa akiwemo Rais Xi Jinping na kuweka mipango mingi ambayo italeta mabadiliko ya kweli katika maisha ya wazimbabwe.

    Mipango hiyo inalenga zaidi ujenzi wa barabara, reli, usafiri wa anga na miradi ya mabwawa ya uzalishaji wa nishati ya umeme.

    Rais Mnangagwa aliongeza kuwa mikataba mingi ya makubaliano ilisainiwa kati ya nchi hizo mbili ili kuendeleza ushirikiano wa kiuchumi, maendeleo ya utaalamu, elimu na maeneo mengine ya kiuchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako