• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kuna nini nyuma ya Marekani katika vita ya kibiashara dhidi China? Sio kuhusu pengo la kibiashara

  (GMT+08:00) 2018-04-08 17:34:44

  Serikali ya Rais Trump inataka kutatua tatizo la Marekani kuwa na pengo kwenye biashara kati yake na China, ambalo wamesema linaligharimu taifa la Marekani mamia ya mabilioni ya dola za kimarekani kwa mwaka. Ndiyo maana Rais Trump anaongoza nchi yake kwa vita ya kibiashara yenye gharama na uharibifu mkubwa dhidi ya mshirika wake mkubwa zaidi wa kibiashara na nchi ya pili kwa ukubwa wa uchumi duniani.

  Walau ndilo jambo ambalo wamekuwa wakimwambia kila mtu. Lakini kutokana na mvutano kuendelea, sasa imekuwa wazi kuwa Marekani inachoona kuwa ni tatizo, ni ukuaji wa nguvu ya ushindani kutoka China, na changamoto ambayo China inatoa kwa Marekani yenye hadhi ya kuwa taifa lenye nguvu duniani.

  Tozo ya ushuru wa wenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 50 dhidi ya bidhaa kutoka China ukilenga zaidi sekta zinazohusiana na mpango wa 'Made in China 2025' ambao unalenga kukuza zaidi sekta ya uzalishaji ya China.

  Hakuna jambo lisiloeleweka kwa nchi kujiwekea mpango wa maendeleo. Kama ilivyo China kuwa na 'Made in China 2025', Ujerumani wana mpango wao wa 'industry 4.0'. Hata Marekani pia walikuwa na mpango wao chini ya Rais Barack Obama kufufua tena sekta ya uzalishaji.

  Lakini serikali ya Trump inaonekana kutaka kuingia ushindani na China. Kwa nini? Kwa sababu, kama utafanyika kwa ufasaha, China itaipiku Marekani katika mbio hizo na kutawala zaidi kwenye sekta zinazoibuka hivi karibuni kama vile matumizi ya akili bandia (AI) na matumizi ya roboti.

  Kwa muono wa Trump, kuendelea kukua kiuchumi kwa China ni tishio kwa Marekani linalopaswa kudhibitiwa. Mtazamo huo ulidhihirika katika mkakati wa kwanza wa usalama wa serikali ya Trump, ambao ulitambua China kama mshindani wa kimkakati. Serikali ya Trump inaonekana kutaka kuizuia China kujiendeleza kwa njia ya amani kwa kuhujumu upanuzi wa uchumi wake. Swali ni; Je wataweza?

  Haiwezekani. China tayari ina akiba kubwa zaidi duniani ya fedha za nje. Idadi ya watu wenye kipato cha kati wa China imeizidi ile ya Marekani ikifanikiwa kuwa kubwa zaidi duniani mwaka 2015.China imekadiriwa kuwa itaipita Marekani kwa kuwa na soko kubwa zaidi la rejareja la ndani mwaka huu. Na huko Shanghai mwezi Novemba, China itaandaa mkutano wa kimataifa wa kwanza kuwahi kufanyika kuhusu Biashara ya Uuzaji na Ununuaji nje ya nchi, ambao ni alama kubwa inayoonyesha azimio la nchi hiyo ya kufanya mageuzi na kufungua mlango, na kuimarisha uhusiano wake na nchi nyingine duniani.

  Kutokana na ukubwa wake, idadi ya watu wake, na kufanya uchumi wa kisasa wenye ustaarabu, China imefanikiwa kuyazuia makelele ya Marekani yanayovuma kupitia Bahari ya Pasifiki. Licha ya serikali ya Trump kuendeleza sera yake ya kujilinda na kujitenga, China itaendelea mbele na maendeleo yake, ikiwemo mpango wa 'Made in China 2025'.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako