• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vijiji 1,705 vyaondokana na umaskini mwaka jana mkoani Tibet

    (GMT+08:00) 2018-04-08 18:18:02

    Mwaka jana, maendeleo makubwa yalipatikana katika kuondoa umaskini mkoani Tibet, China, na kuanzia mwaka 2015 hadi mwishoni mwa mwaka jana, watu laki 2.6 wameondokana na umaskini.

    Mwaka huu, mkoa unaojiendesha wa Tibet utatenga Yuan bilioni 11.7 sawa na dola za kimarekani bilioni 1.8 ili kuwafanya watu wengine zaidi ya laki 1.5 kuondokana na umaskini. Katika siku za baadaye, Tibet itaweka kipaumbele kwenye kazi za kuondoa umaskini katika sehemu zenye umaskini uliokithiri mkoani humo, na kujitahidi kuelekeza pesa, kwenye miradi na watu wenye vipaji katika sehemu hizo.

    Habari nyingine zinasema mkoa wa Tibet unatoa huduma za bure za upimaji wa kimwili kwa wakazi na watawa. Hii ni miaka ya 7 mfululizo kwa mkoa huo kutoa huduma hizo. Mwaka jana watu milioni 3 walifanyiwa kwa bure upimaji wa kimwili mkoani humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako