• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Syria yakana kujihusisha na matumizi ya silaha za kikemikali Ghouta Mashariki

    (GMT+08:00) 2018-04-09 08:50:08

    Serikali ya Syria imekana kujihusisha na matumizi ya silaha za kikemikali kwenye eneo la Ghouta Mashariki, na kusema shutuma hizo ni maneno matupu yasiyothibitika. Ofisa wa wizara ya mambo ya nje ya Syria amesema kila wakati jeshi la Syria linapopata maendeleo kwenye mapambano dhidi ya ugaidi, kunakuwa na shutuma zisizo na msingi dhidi yake, ambazo lengo lake ni kutafuta kisingizio cha kuwapa magaidi nafasi ya kujiokoa. Kabla ya hapo, nchi za magharibi zilionya kuwa kama jeshi la Syria likithibitishwa kuwa limetumia silaha za kikemikali kwenye eneo la Ghouta Mashariki, zitalichukulia hatua za kijeshi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako