• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa kutuma wataalamu nchini Iraq kukusanya ushahidi wa uhalifu wa kundi la IS

    (GMT+08:00) 2018-04-09 09:01:03

    Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Miguel de Serpa Soares amesema Umoja wa Mataifa utatuma wataalamu nchini Iraq kukusanya ushahidi wa uhalifu uliotendwa na kundi la Islamic State.

    Akiongea mjini Baghdad baada ya kukutana na waziri wa mambo ya nje wa Iraq Ibrahim al-Jaafari, Bw. Soares amesema wataalamu waliotumwa na Umoja wa Mataifa watashirikiana na serikali na idara za sheria za Iraq kukusanya ushahidi wa uhalifu wa kundi la IS. Umoja wa Mataifa pia utaendelea kuunga mkono ukarabati wa Iraq na kulinda usalama na utulivu wa nchi hiyo.

    Ofisa mmoja wa wizara ya mambo ya nje ya Iraq amesema, Bw. Soares na Bw. Jaafari pia wamejadili njia halisi za kukusanya ushahidi, ikiwemo kwenda kwenye maeneo yaliyoshambuliwa na kundi la IS na kuwatembelea waathirika. Iraq imesema itakabidhi taarifa ilizonazo kwa wataalamu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako