• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la Misri lawaua magaidi 4 huko Sinai

    (GMT+08:00) 2018-04-09 09:16:36

    Msemaji wa jeshi la Misri ametangaza kuwa jeshi la Misri limewaua magaidi wanne kwenye operesheni ya kupambana na magaidi katika peninsula ya Sinai.

    Mapambano hayo yamesababisha vifo vya magaidi 167 na askari 24 tangu kampeni ya jumla ya kupambana na ugaidi ianze mwezi Februari.

    Jeshi hilo pia limewakamata magaidi 250 na kutegua mabomu 30, na kuharibu maficho 386 ya magaidi na kukamata mabomu 16.

    Eneo la Sinai Kaskazini linalopakana na Isarel na ukanda wa Gaza limekuwa kiini cha mapambano na kusababisha vifo vya mamia ya wanajeshi na polisi, tangu aliyekuwa rais wa Misri Mohamed Morsi kuondolewa madarakani mwaka 2013.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako