• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la Nigeria lawakomboa mateka 149 kutoka kwa Kundi la Boko Haram

    (GMT+08:00) 2018-04-09 09:17:59

    Jeshi la Nigeria limesema limewaua waasi watano wa kundi la Boko Haram katika jimbo la Borno, kaskazini mashariki mwa Nigeria, na kuwaokoa mateka 149.

    Msemaji wa jeshi la Nigeria Bw. Nwachukwu ametoa taarifa akisema, jeshi la Nigeria lilifanya operesheni ya kuwaondoa waasi waliosalia wa kundi la Boko Haram karibu na ngome yake kuu ya zamani iliyoko kwenye msitu wa Sambisa, ambapo waasi watano waliuawa na wengine watano wamekamatwa, na mateka 149 wameokolewa.

    Msemaji huyo ameongeza kuwa kati ya mateka hao 149 kuna wanawake 54 na watoto 95, ambao hivi sasa wamepelekwa katika kituo cha afya kwa ajili ya matibabu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako