• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjumbe maalumu wa UN aahidi juhudi zaidi kuhimiza mazungumzo ya amani ya Yemen

    (GMT+08:00) 2018-04-09 09:26:46

    Mjumbe mpya maalumu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia mgogoro wa Yemen Bw. Martin Griffiths, ambaye yuko ziarani nchini Oman amesema, atahimiza mazungumzo ya amani kati ya pande zinazopambana nchini Yemen, ili wafikie maafikiano. Lakini pia amekiri kuwa si rahisi kutimiza lengo hilo.

    Bw. Griffiths amesema baada ya kufanya ziara nchini Saudi Arabia na Yemen, anaona pande zote zina matumaini ya kutimiza amani, kuanzisha mazungumzo na kukomesha balaa kwa watu.

    Amesisitiza kuwa wananchi wanatakiwa kuamua mustakabali wa nchi yao, lakini haimaanishi kuwa misaada inayotolewa na nchi nyingine haisaidii. Nchi jirani za Yemen pia zinatumai kuwa Yemen itapata utulivu na ustawi, na kuishi pamoja na nchi jirani zake kwa amani.

    Amedokeza kuwa mazungumzo kati yake na pande zinazohusika yamepata maendeleo makubwa, na atawasilisha ripoti kuhusu ziara zake kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ndani ya siku 10.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako