• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka, Kombe la CAF: Klabu za tatu za Afrika Mashariki Zapata ushindi

    (GMT+08:00) 2018-04-09 10:51:03

    Timu tatu za Afrika Mashariki, Rayon Sport ya Rwanda, Gor Mahia ya Kenya na Young Africans ya Tanzania jana zimepata ushindi katika mechi zake za kwanza za hatua ya mtoano kwenye michuano ya kombe la shirikisho ngazi ya vilabu.

    Rayon ilipata ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Costa Do Sol ya Msumbiji, yaliyofungwa na Hussein Shaban aliyefunga mawili na moja likifungwa na Kevin Muhire.

    Nako kwenye kaunti ya Machakos nchini Kenya, wenyeji Gor Mahia walipata ushindi wa goli moja kwa sifuri dhidi ya timu ya supersport United kutoka Afrika Kusini.

    Kwa upande wao Yanga ya Dar es Salaam walipata ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya wageni wao Wolaitta Ditcha Kutoka Ethiopia, kwa magoli yaliyofungwa na Emmanuel Martin pamoja na Raphael Daudi.

    Ili kujihakikishia nafasi ya kufuzu hatua ya makundi, timu hizo zitalazimika kulinda ushindi wake kwenye mechi za marudiano na wapinzani wao hao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako