Kwa mara nyingine tena, dereva Sebastian Vettel wa Ujerumani ameshinda taji la mbio za langalanga la Bahrain zilizofanyika jana ikiwa ni mara ya 200 kwa dereva huyo kuwahi kushiriki mbio za magari.
Ushindi huu ni wa pili mfululizo kwa dereva huyo wa timu ya ferari tangu kuanza kwa msimu wa mwaka 2018 akiwa tayari ameshinda taji la Australia mapema mwezi Machi.
Mshindi wa pili katika mbio hizo alikuwa Valterri Botas wa Finland akifuatiwa na mwenzake katika timu ya Mercedes Lewis Hamilton wa Uingereza.
Vettel ambaye ni bingwa mara nne wa michuano ya magari, yeye pamoja na Lewis Hamilton wanawania kufikisha rekodi ya ubingwa mara tano.
Baada ya kukamilika kwa mbio hizo za Bahrain madereva wanaoshiriki mbio hizo wanaanza kujiandaa kwa ajili ya mbio za China zitakazofanyika Aprili 18 mjini Shanghai.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |