• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa wakuu wa vyombo vya habari vya Asia wafanyika mkoani Hainan China

    (GMT+08:00) 2018-04-09 13:25:36

    Mkutano wa wakuu wa vyombo vya habari vya Asia umefanyika leo mjini Sanya, mkoani Hainan. Mkuu wa Idara ya matangazo ya Kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China Bw. Huang Kunming amehudhuria ufunguzi wa mkutano huo, akitoa hotuba ya "kuonesha moyo wa kufungua mlango na kufanya uvumbuzi, kuhimiza kwa pamoja ustawi na maendeleo barani Asia".

    Bw. Huang Kunming ameeleza kuwa, mwaka huu ambayo ni miaka ya 40 tangu China itekeleze sera ya mageuzi na kufungua mlango, China inapenda kushirikiana na Asia na dunia nzima kuendelea kutafuta njia ya kufanya uvumbuzi na kunufaishwa kwa pamoja na matokeo ya maendeleo yaliyopatikana. Rais Xi Jinping ametoa nadharia muhimu na mapendekezo yanayohusu mustakabali wa binadamu, na kuhimiza maendeleo ya amani ya dunia na ustawi wa Asia.

    Watu zaidi ya 300 wakiwemo wakuu 140 wa vyombo muhimu vya habari kutoka nchi 40 barani Asia pamoja na wataalamu wa utamaduni wa Asia na wajumbe kutoka pande zinazohusika walihudhuria ufunguzi wa mkutano huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako