• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China ina imani kukabiliana na mvutano wa kibiashara kati yake na Marekani

    (GMT+08:00) 2018-04-09 16:32:04

    Rais Donald Trump wa Marekani jana usiku alitoa taarifa kwenye mtandao wa kijamii akisema, ingawa mgogoro wa kibiashara umetokea kati ya China na Marekani, lakini rais Xi ni rafiki yake mkubwa na nchi hizo mbili zitakuwa na siku nzuri za mbele. Kauli hiyo imeifanya jumuiya ya kimataifa kujiuliza kama rais Trump atajisalimisha kwa China? Na je, vita vya kibiashara kati ya nchi hizo mbili vitaisha?

    Kwa mujibu wa maoni ya Marekani yanayobadilika tangu nchi hiyo kuzusha mgogoro wa kibiashara dhidi ya China, watu hawana matarajio makubwa kwa taarifa hiyo ya rais Trump. Hatua ya kulipiza kisasi inayochukuliwa na China haitarajiwi na Marekani na imesababisha tofauti ya maamuzi ya ndani ya Marekani. Lakini mpango huo wa kuzuia maendeleo ya China na kulinda umwamba wa Marekani uliodumu kwa muda mrefu hautalegea ndani ya muda mfupi. Uwezekano mkubwa ni kwamba Marekani itaendelea kutumia mkakati wa kuisumbua China na kutafuta fursa ya kuishambulia.

    Tangu mwezi wa Agosti mwaka jana, Marekani ilipoanzisha uchunguzi kwa kutumia kipengele cha 301 cha sheria ya biashara ya Marekani dhidi ya China, nchi hiyo imeanza kuitishia China kwa kutumia vikwazo huku ikitoa ishara ya kutaka kufanya mazungumzo na China, ili kuilazimisha China kusalimu amri. Lakini China inaendelea kuzidisha mkakati wa mageuzi na ufunguaji mlango na kutoongozwa na misimamo inayobadilika ya Marekani. China inatekeleza kithabiti sera zilizowekwa ili kukabiliana na uchokozi wa Marekani na ina imani ya kushinda katika vita vya kibiashara.

    Mkutano wa mwaka 2018 wa baraza la Asia la Boao umefunguliwa, na rais Xi Jinping wa China anatarajiwa kutoa hotuba na kutangaza hatua mpya za mageuzi na ufunguaji mlango wa duru mpya ili kujenga "Asia yenye uwazi na uvumbuzi na Dunia yenye ustawi na maendeleo". China sio tu inazingatia maendeleo yake yenyewe, bali pia inapenda kushirikiana na sehemu mbalimbali duniani kukumbatia amani, maendeleo na ustawi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako