• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wasomi wasema Asia itaendelea kuwa kanda yenye kasi kubwa zaidi ya ukuaji wa uchumi duniani

  (GMT+08:00) 2018-04-09 16:32:11

  Mkutano wa mwaka wa Baraza la Asia la Bo'ao unaendelea kufanyika huko Bo'ao, mkoani Hainan, China. Wasomi wengi wa ndani na nje ya China wamesema katika miaka 20 ijayo, Asia itaendelea kuwa kanda yenye kasi kubwa zaidi ya ukuaji wa uchumi duniani, na hatua mpya za kufungua mlango kwa nje zitakazotangazwa na China kwenye mkutano huo pia zinafuatiliwa.

  Kwenye kongamano la "makadirio ya uchumi wa Asia" kando ya mkutano huo, aliyekuwa gavana wa Benki Kuu ya China Dai Xianglong amesema katika miaka 20 ijayo na hata hadi miaka ya 50 ya karne hii, Asia itakuwa kanda yenye kasi kubwa zaidi ya ukuaji wa uchumi duniani. Anasema,

  "katika miaka 20 iliyopita, kiwango cha wastani cha ongezeko la uchumi wa Asia kwa mwaka ni asilimia 6.8, na inatarajiwa kuwa kiwango hicho kitaendelea kuwa juu zaidi duniani katika miaka 20 ijayo. Sababu moja kuu ni maendeleo yenye nguvu ya China, na kasi ya ukuaji wa uchumi wa India itakuwa kubwa zaidi, ushirikiano kati ya China, Japan, Korea Kusini na nchi kumi za Jumuiya ya Nchi za Kusini Mashariki mwa Asia utaimarika zaidi, na maendeleo ya 'Ukanda Mmoja, Njia Moja' yataipatia Asia fursa mpya."

  Akizungumzia mustakbali wa uchumi wa China, Bw. Dai amesema katika miaka ya hivi karibuni, kasi ya ongezeko la uchumi wa China inapungua, lakini hii haimaanishi kuwa uchumi unashuka chini, bali ni kutokana na China kurekebisha mkakati wa maendeleo ya uchumi kwa hiari na ufanisi. Anaona kuwa katika siku zijazo, China itaangalia zaidi ubora wa maendeleo ya uchumi wake. Anasema,

  "Kwanza ni kufanya mageuzi kwenye sekta ya utoaji bidhaa, na kupunguza uwezo wa uzalishaji unaokiuka sheria na kanuni, na kujenga uwezo wa uzalishaji unaotumia teknolojia ya kisasa na ya hali ya juu. Pili kuboresha utoaji wa fedha, kuinua uwezo wa jamii kukusanya fedha. Tatu ni kuboresha utoaji wa nyumba za kuishi, na kuzuia kuporomoka kwa soko la nyumba."

  Anaona kuwa hatua hizo zitasaidia uchumi wa China kuendelezwa kwa utulivu.

  Kwenye mkutano huo, ni hatua gani mpya za mageuzi na ufunguaji mlango zitakazotangazwa na China pia inafuatiliwa na nje. Katibu mkuu wa Vyama vya Viwanda na Biashara vya India FICCI Bw. Sanjaya Baru anasema,

  "Kwa mujibu wa upande wa maendeleo, kutokana na kuinuka kwa uwezo wa matumizi ya wachina na kuongezeka kwa mapato ya raia, China itakuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kuagiza bidhaa kutoka nchi nyingine zikiwemo nchi zinazoendelea. Kama China itafanya kazi kubwa zaidi katika kupanua uagizaji bidhaa kutoka nje na kuwekeza nje ya nchi, itakuwa ni jambo zuri kwa China na nchi zinazoendelea."

  Wasomi wanaoshiriki kwenye kongamano hilo pia wamesema ukuaji wa uchumi wa Asia bado unakabiliwa na hali ya kukosekana kwa uhakika, ukiwemo mgogoro wa kibiashara unaoendelea kati ya China na Marekani. Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi wa Raia ya China Fan Gang anasema,

  "Watu wanasema China inauza bidhaa nyingi nchini Marekani, lakini kutengeneza bidhaa hizo kunaihitaji China kuagiza bidhaa kutoka nchi nyingine za Asia, kama vile vioo vya Korea Kusini na vipuri vya Japan na Malaysia, pamoja na bidhaa nyingine za rasilimali kutoka nchi mbalimbali za Asia Kusini Mashariki. Mgogoro kati ya China na Marekani utaathiri mnyororo mzima wa biashara."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako