• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 14 wauawa katika shambulizi la kombora nchini Syria

    (GMT+08:00) 2018-04-09 16:57:20

    Watu 14 wakiwemo askari wa kikosi cha Iran wanaoshirikiana na jeshi la serikali ya Syria wameuawa katika shambulizi la kombora lililolenga kambi ya jeshi la anga iliyoko mkoani Homs katikati ya Syria alfajiri ya leo.

    Shambulizi hilo limekuja wakati jumuiya ya kimataifa ikizozana kuhusu tuhuma za jeshi la Syria kutumia silaha za kemikali katika shambulizi dhidi ya waasi katika wilaya ya Douma, eneo la Ghouta Mashariki mjini Damascus.

    Bado haijafahamika shambulizi la leo alfajiri lilifanywa na nani, lakini vyombo vya habari vya Syria vinasema huenda shambulizi hilo limefanywa na Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako