• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa mwito kwa Russia na Marekani kutatua migongano kupitia mazungumzo ya kirafiki

    (GMT+08:00) 2018-04-09 18:15:06

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema, China inatoa mwito kwa Russia na Marekani kutatua migongano kupitia mazungumzo ya kirafiki juu ya msingi wa usawa na kuheshimiana na kufuata uhusiano wa kimataifa unaotambuliwa na jumuiya ya kimataifa na kanuni za sheria za kimataifa.

    Hivi karibuni Marekani ilitangaza kuwa, imeamua kuweka vikwazo dhidi ya watu 24 na mashirika 14 ya Russia kutokana na vitendo mfululizo vya kuharibu demokrasia ya magharibi vinavyofanywa na Russia, nayo wizara ya mambo ya nje ya Russia imetoa taarifa ikisema itajibu kithabiti vikwazo vipya vya Marekani.

    Bw. Geng amesema, China siku zote inapinga matumizi ovyo ya vikwazo au kutoa vitisho kwenye uhusiano wa kimataifa. Amesisitiza kuwa Russia na Marekani zote ni nchi muhimu zenye ushawishi mkubwa duniani na nchi wajumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na zinabeba majukumu muhimu kwa amani na usalama wa dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako