• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Bei ya bidhaa na uchukuzi yapanda Rwanda

    (GMT+08:00) 2018-04-09 18:27:50

    Bei ya bidhaa na ile ya usafiri imepanda nchini Rwanda na sasa wakaazi huenda wakahitaji kutumia fedha zaidi kwa huduma na bidaa za matumizi ya kila siku.

    Mamlaka ya kuratibu bei ya usafiri nchini humo (Rura) imeongeza nauli ya mabasi kufikia kati ya franc 1 na franc 400 kwa wale wanaosafiri nje ya mjimkuu Kigali.

    Mamlaka hiyo imesema kuongezewa kwa bei hiyo kunatokana na kupanda kwa gharama za oparesheni.

    Imetaja gharama hizo kama bima na kuongezeka kwa bei ya mafuta.

    Sasa lita moja ya petroli imeongezeka hadi dola 1.21 kutoka bei ya mwaka 2015 ya dola 1.02 huku nayo dizeli ikifikia dola 1.19.

    Kutokana na kupanda kwa mafuta, gharama ya uchukuzi pia imeongezeka kwa bidhaa za kilimo na zile za viwandani na hivyo ongezeko la jumla kusambaa hadi kwa wateja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako