• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Wakulima wa kahawa waonywa wasiuza nje ya mfumo uliowekwa

    (GMT+08:00) 2018-04-09 18:28:16

    Chama Kikuu cha Ushirika cha Mkoa wa Kagera cha wauza kahawa (KCU),nchini Tanzania kimeibuka na kutoa onyo kwa wakulima watakaouza zao hilo nje ya mfumo mpya uliowekwa

    KCU imeonya kuwa wakulima watakaofanya hivyo watakabiliana na adhabu ya kutaifishwa kwa mazao yao.

    Mwenyekiti wa Bodi ya KCU, Onesmo Niyegila alisema kuwa utaratibu wa sasa ni kwa kahawa yote kukusanywa kupitia kwenye vyama vya ushirika na kupelekwa sokoni mjini Moshi ambapo wanunuzi wote watanunulia hapo mnadani.

    Kuhusu bei ya kahawa, Niyegila alisema malipo ya awali yaliyopendekezwa na menejimenti na bodi ya chama hicho katika mkutano mkuu uliofanyika Machi 27 ni Sh 1,000 kwa kilo ya kahawa ya maganda.

    Hata hivyo, baada ya mjadala wanachama waliagiza kupitiwa upya kwa makisio hasa kwa upande wa malipo ya awali na kuangalia namna ya kupandisha kiwango cha malipo ya wali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako