• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi za Afrika zatakiwa kuzalisha mazao ya jadi ili kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa

    (GMT+08:00) 2018-04-10 08:53:05

    Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa mataifa FAO limezitaka nchi za Afrika kuzalisha mazao ya jadi hasa yale yanayohimili ukame, ili kukabiliana na madhara ya mabadiliko ya hali ya hewa.

    Akiongea na wanahabari mjini Nairobi, Ofisa anayeshughulikia mazao wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa mataifa Bw. Wilson Ronno, amesema utafiti umeonyesha kuwa Afrika itapoteza sehemu kubwa ya ardhi inayolimika kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.

    Bw. Ronno amekumbusha kuwa nchi za Afrika zinatakiwa kuhimiza kilimo cha uwele, mtama, muhogo na mboga za majani za maeneo ya Afrika kwa kuwa mazao hayo yanaweza kuhimili ukame.

    Amesema kutokana na maendeleo yanayopatikana barani Afrika, wakazi wa mijini wanaonekana kutumia zaidi chakula kinachoagizwa kutoka nje, na kuacha kutumia chakula kinachozalishwa ndani. Matokeo yake ni kuwa wakulima hawana motisha wa kuzalisha mazao ya jadi kama uwele na mtama.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako