• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • FAO latahadharisha dhidi ya tishio la usalama wa chakula kanda ya Asia na Pasifiki

    (GMT+08:00) 2018-04-10 09:25:00

    Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO limetahadharisha kuwa kama nchi za kanda ya Asia na Pasifiki hazitachukua hatua mara moja kupunguza athari za mabadiliko ya hali ya hewa kwa kilimo, huenda zitakabiliwa na tatizo la usalama la chakula.

    Kwenye mkutano wa 34 wa FAO kanda ya Asia na Pasifiki uliofanyika nchini Fiji, imefahamika kuwa katika miaka ya karibuni uchumi wa kanda hiyo ulikua kwa kasi, lakini maendeleo madogo yamepatikana katika kukabiliana na suala la njaa kwenye kanda hiyo, ambako watu milioni 500 bado wanakabiliwa na njaa na utapia mlo, hali ambayo itatatiza juhudi za Umoja wa Mataifa za kutimiza lengo la kutokomeza njaa kabla ya mwaka 2030.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako