• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Algeria yatoa wito kwa nchi za Afrika kushirikiana kuyakatia vyanzo vya fedha makundi ya kigaidi

    (GMT+08:00) 2018-04-10 09:43:58

    Waziri wa mambo ya nje wa Algeria Bw. Abdelkader Messahel ametoa wito kwa nchi za Afrika kushirikiana kuandaa mkakati wa pamoja wa kukata vyanzo vya fedha kwa makundi ya kigaidi.

    Akishiriki kwenye mkutano wa ngazi ya juu wa kuyakatia vyanzo vya fedha makundi ya kigaidi barani Afrika uliofanyika mjini Algiers, Bw. Messahel amesema makundi ya kigaidi yanapata pesa kutokana na biashara ya dawa za kulevya, magendo ya silaha, watu, utekaji nyara na kutengeneza pesa bandia. Amependekeza nchi za Afrika kuongeza mawasiliano na kutoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuendelea kuongeza ushirikiano na nchi za Afrika ili kuzuia vyanzo vya fedha kwa makundi ya kigaidi.

    Wajumbe kutoka Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika, Umoja wa Ulaya na mashirika mengine ya kimataifa wameshiriki kwenye mkutano huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako