• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Michezo ya Jumuiya ya Madola: Uganda yaongeza medali ya dhahabu, yashinda shaba pia.

  (GMT+08:00) 2018-04-10 10:27:28

  Timu ya Uganda inayoshiriki michezo ya jumuiya ya madola nchini Australia imefanikiwa kuongeza medali nyingine ya dhahabu kufuatia ushindi wa nafasi ya kwanza aliopata Stella Chesang kwenye mbio za mita 10000 wanawake.

  Katika mbio hizo, Uganda ilipata medali nyingine kupitia Mercyline Chellangat alishinda nafasi ya tatu na kutwaa medali ya shaba na kuifanya timu ya Uganda iwe na jumla ya medali tatu kwenye mashindano hayo.

  Nafasi ya pili katika mbio hizo za wanawake ilitwaliwa na mwanariadha mwingine kutoka Afrika Mashariki, Stacy Ndiwa aliyepata medali ya fedha.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako