• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa fedha wa Kenya asema hatua za Marekani za kujilinda kibiashara zitahujumu maslahi yake yenyewe

    (GMT+08:00) 2018-04-10 14:10:20

    Waziri wa fedha na mipango wa Kenya Bw. Henry Rotich amesema kama Marekani ikiendelea kuchukua hatua za kujilinda kibiashara,itajihujumu yenyewe, na pia kuleta athari mbaya kwa uchumi wa dunia.

    Bw. Henry Rotich ameeleza wasiwasi kutokana na kupamba moto kwa mgogoro wa kibiashara kati ya China na Marekani, akisema:

    "Hatua hizi za Marekani zinarudisha nyuma dunia yetu. Mpango wa pande nyingi wa kuondoa vizuizi vya kibiashara na vya ushuru utaweza tu kutekelezwa kihalisi katika nchi za Asia na Afrika endapo kila nchi itafungua soko lake kwa nje chini ya mfumo wa WTO. Ufunguaji mlango ndio unaoongeza nguvu yetu ya ushindani, kama hakuna ushindani wa haki, basi hatua za kuzuia biashara dhidi ya nchi nyingine hatimaye zitajihujumu tu. Hatua ya kuongeza ushuru wa forodha kwa bidhaa za nchi nyingine, inamaanisha kuwa wateja wa Marekani watalipa gharama kubwa zaidi, Marekani inadhani kuwa inafanya hivyo kulinda watengenezaji bidhaa wenyeji, lakini kwa kweli hakuna watakaonufaika na sera hiyo. Tunapaswa kuacha kabisa sera za kujilinda kibiashara. Dunia ya leo imekuwa tofauti sana na ile ya zamani, kila nchi inajitahidi kujiendeleza kiuchumi, lakini ni hakika kwamba sera za kujilinda kibiashara zitaleta athari hasi kwa maendeleo ya uchumi, na kamwe haziwezi kufikia lengo lililotarajiwa."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako