• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Jamhuri ya Kongo ahimiza ushirikiano kati ya nchi yake na China kufikia ngazi mpya

    (GMT+08:00) 2018-04-10 18:00:39

    Rais wa Jamhuri ya Kongo Bw. Denis Sassou Nguesso amesema anapenda kuhimiza ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya nchi yake na China kufikia ngazi mpya.

    Rais Sassou Nguesso amesema hayo alipopokea hati za utambulisho za balozi mpya wa China nchini Jamhuri ya Kongo Bw. Ma Fulin. Ameongeza kuwa mwaka 2016, marais wa nchi hizo mbili waliamua kuboresha uhusiano kati ya nchi hizo mbili kuwa wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote ambao umepata maendeleo zaidi.

    Kwa upande wake, Balozi Ma Fulin amesema kuwa katika miaka ya hivi karibuni, chini ya msukumo wa marais wa nchi hizo mbili, uhusiano kati ya China na Jamhuri ya Kongo umeendelezwa vizuri na kupata matokeo mazuri. Ameongeza kuwa atahimiza utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa kati ya marais wa nchi hizo mbili na kuimarisha zaidi ushirikiano wa kimkakati kati ya China na Jamhuri ya Kongo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako