• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania yaongoza mitambo ya kisasa ya umeme EAC

  (GMT+08:00) 2018-04-10 19:22:12

  TANZANIA ni nchi pekee katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) inayotumia mitambo ya kisasa ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia (combined cycle).

  Mitambo hiyo ina uwezo wa kuchoma gesi hiyo na kuzalisha umeme pamoja na kutumia mvuke wake, kuzalisha megawati nyingine.

  Nchi ina mitambo sita ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia, miwili ikiwa na mitambo hiyo ya kisasa ya kutumia mvuke pia kuzalisha umeme, ambayo inasaidia kuzalisha umeme zaidi kuliko mitambo ya kawaida.

  Meneja miradi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Stephen Manga amesema mitambo hiyo ya kisasa iliyozinduliwa hivi karibuni na Rais John Magufuli katika mradi wa kufua umeme wa Kinyerezi II, ina uwezo wa kuzalisha Megawati 240.

  Akizungumzia mpango wa serikali kuuza umeme katika nchi za Afrika Mashariki, katika mradi wa msongo wa kilovoti 400 kwa umbali wa kilometa 414, alisema tayari wakandarasi wanaendelea na utekelezaji wa mradi wa kuunganisha umeme kutoka Singida, Manyara mpaka nchini Kenya.

  Umekamilika siku 45 kabla ya muda uliopangwa, kutokana na serikali kutoa Sh bilioni 120 na mkopo wa gharama nafuu kutoka Japan wa dola za Marekani milioni 292.4 na kufanya mradi huo kugharimu dola za Marekani milioni 344 sawa na Sh bilioni 758.

  zaidi ya asilimia 50 ya umeme unaozalishwa nchini unatokana na nishati ya gesi asilia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako